UTARATIBU MPYA WA UENDESHAJI  WA ELIMU YA KIISLAMU KWA POSTA

 

1.0 Utangulizi:

 

Ili kkupunguza  gharama kwa wasomaji na kuongeaa ufanisi imelazimu kufanya mabadiliko katika uendeshaji wa Elimu ya kiislamu kwa Posta (E.K.P) katika mabadiliko haya Juzuu 24 za E.K.P. zimechanganywa na kutolewa kwa muhutasari katika Juzuu 7 zenye anwani ya  “Darasa la Watu Wazima.” juzuu hizi  7 ukiziandanisha na juzuuu 24 za E.K.P. zinawiana kama zinavyoonekana katika jedwali lifuatalo:

 

Juzuu

Daresa La Watu Wazima

Juzuu za E.K.P.

1.

Lengo la Maisha ya Mwanadamu

Jz. 1,2,3,5-10

2.

Nguzo za uislamu

Jz 11-15

3.

Qur-an na Sunnah

Jz 4,18,19

4.

Familia ya Kiislamu

Jz. 16

5.

Jamii ya Kiislamu

Jz. 17

6.

Historia ya Kuhuisha Uislamu

Jz. 20-23

7.

Kuhuisha Uislamu katika Jamii

Jz. 24

 

Pamoja na mabadiliko haya maudhui na lengo la E.K.P. Linabakia pale pale. Hivyo, tunawaomba na kuwataka radhi wale waliokwisha jiunga na E.K.P. kuwa wajiandikishe upya kufuata utaratibu huu mpya.

 

2.0 Lengo la E.K.P.

  2.1 Malengo ya jumla:

a)      Kuwawezwasha wasomaji kuusimamisha Uislamu katika jamii na kuutekeleza vilivyo katika kila kipengele cha maisha yao.

 

b)      Kuwaandaa wanafunzi wa secondary kwa mtihani wa kidato cha nne(CSEE) wa Elimu ya Dini ya Kiislamu, hasa wale wasiopata fursa ya kufikiwa na Waallimu wa somo hili.

 

c)      Kuwaandaa walinganiaji wa Uislamu na Waalimu wa somo la Elimu ya Dini ya Kiislamu kwa shule za Msingi na Secondari.

 

   2.2  Malengo Makhsusi:

 

Ni matarajio yetu kuwa wale watakao hitimu masomo haya  ya E.K.P, wataweza.

a)      Kueleza mtazamo sahidi juu ya elimu, dini, lengo na hadhi ya mwanadamu hapa ulimwenguni.

 

b)      Kuainisha sifa za waumini wa kweli kwa mujibu wa Quruani  na sunna.

 

c)      Kuutetea Uislamu kwa hoja  madhubuti na kuonyesha kuwa ndio dini pekee inayostahiki na kila mwenye akili na busara.

 

d)      Kutekeleza  vilivyo nguzo tano za Uislam na kufikialengo tarajiwa.

 

e)      Kueleza namna ya kumuabudu  Allahn (S.W) katika kila kipengele cha maisha yao ya binafsi, familia na jamii.

 

3.0 Kujisajili  kwa E.K.P

 

Chukua fomu ya kujisajili kuwa mwanafunzi wa E.K.P. kwenye vituo mbalimbali katika miji ya Tanzania vitakavyo tangazwa. gharama ya kila fomu ni Tsh. 1000/= (kwa wanafunzi Tsh. 200/=)

 

Jaza fomu hiyo na kuituma kwa Mwalimu mratibu S.L.P. 55105, Dar es Salaam, Simu 022-2450069/0744 369935. Ambatanisha  fomu hiyo na picha tatu (3) za rangi za ukubwa wa “pass port”. utapewa namba ya usajili na kitambulisho rasmi cha mwanafunzi wa E.K.P.

 

4.0 Upatikanaji wa Juzuu za Masomo

 

  4.1 Msomaji atanunua juzuu za “Darasa la watu wazima “ kwenye maduka ya vitabu    au vituo mbalimbali mikoani vitakavyo tangazwa.

 

  4.2   Bei za juzuu za E.K.P. (Darasa la watu wazima) zinaainishwa katika jedwali lifuatalo:

 

Juzuu

Darasa La Watu Wazima (E.K.P)

Bei

1

Lengo la Maisha ya Mwanadamu

3,000

2

Nguzo za uislamu

4,000

3

Qur-an na Sunnah

2,500

4

Familia ya Kiislamu

2,500

5

Jamii ya Kiislamu

3,000

6

Historia ya Kuhuisha Uislamu

4,000

7

Kuhuisha Uislamu katika Jamii

2,000

Jumla

 

21,000

 

 

  4..3 Kila juzuu itaambatanishwa na bahasha ya maswali ambayo imepigwa muhuri wenye maneno “Usifungue mpaka uwe umesoma na kuelewa”. Bahasha hii ya maswali  atapewa mwanafunzi baada ya kuonyesha kitambulisho chake kwa muhusika kaika kituo au duka la vitabu husika.

 

5.0 Utaratibu wa Usomaji

  5.1 Baada ya kupata juzuu, soma sura kwa makini mara ya kwanza, kisha rudia sura hiyo kwa mara ya pili kwa makini zaidi, kisha fanya zoezi lililotolewa mwisho wa sura. Ikiwa hukuelewa vizuri katika zoezi hilo, rejea tena kusoma  mpaka upate jibu sahihi. Msomaji atafanya hivyo hivyo mpaka amalize sura zote za kitabu husika.

 

  5.2 Baada ya kukisoma kitabu chote na kukielewa vizuri,funguaa bahasha ya maswali ya juzuu hiyo na jibu kutokana na maelekezo,kisha kuyatuma kwa mwalimu mraribu, S.L.P.  55105, Dar es salaam, kwa ajili ya masahihisho. Wakati unangojea majibu ya maswali ya Juzuuu iliyotangulia, endelea kusoma Juzuu inayofuatia/zinazofuatia.

 

  5.3 Mwanafunzi wa E.K.P. atarudishiwa majibu baada ya masahihisho pamoja na ushauri nasaha kulingana na majibu yake. Jumla ya zitachangia asilimia 10(10%) ya tathimini ya mwisho.

 

6.0 Mtihanii wa mwisho

Baada ya kukfibu maswali ya juzuu zote 7 mwanafunzi wa E.K. P. atajiandikisha /atainba  kufanya mtihani wa mwisho ambao utafanyika mwezi wa January na Julai kila mwaka  katika vituo vitakavyotangazwa. Mtihani wa mwisho utuchangia asilimia  90(90%) ya tathimini ya mwisho.   

 

Miezi miwili kabla ya mtihani wa mwisho mwanafunzi wa E.K.P. , Atatakiwa     kufanya mtihani wa “Mock” ambao utamsaidia kujiandaa vizuri kwa ajili ya  mtihani wa mwisho. Mitihani ya “Mock” mwezi Mei na Novemba kila mwaka.

 

7.0 Cheti cha kumaliza Masomo

 

   7.1 Wanafunzi  E.K.P  watakaofaulu vizuri kwa kupata daraja C au zaidi watatunukiwa cheti cha kufaulu masomo ya E.K.P.

 

   7.2 Watakaopata daraja D watashauriwa kurudia mtihani.

 

    7.3 Watakaopata daraja F watakuwa wamefeli na itabidi warudie kozi nzima kwa kufanya tena maswali ya juzuu zote 7, kisha baadaye wafanye tena mtihani kwa kufuata utaratibu wa mitihani ulioelezwa hapo juu.

 

    7.4 Daraja hupatikana kama ifuatavyo:

 

A=81-100,   B=61-80,   C=41-60  D= 40-21,   F=20-0.

 

8.0 Gharama

     8.1 Mwanafunzi wa E.K.P atalazimika kugharamia utumaji wa majibu ya Maswali ya juzuu baada ya kusahihishwa na mwalimu mratibu. Itabidi aambaatanishe maswali hayo na “Post Stamp” zenye dhamani husika.

 

     8.2 Mwanafunzi wa E.K.P. atajiandikisha kwa ajili  ya mtihani wa mwisho na kulipa Tsh. 5000 kama gharama ya mtihani ikiwa ni pamoja na mtihani wa “mock”.

 

Wabillah Taufiq